March 13, 2017
Jina la kiungo Simon Msuva wa Yanga limetajwa na mlinzi wa Zanaco FC ya Zambia, Zio Tembo kuwa ndiye mchezaji aliyewasumbua zaidi na kama wasingekuwa makini basi angewapiga mabao mengi hiyo juzi.

Yanga ilikuwa mwenyeji wa Zanaco kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar na kuisha kwa sare ya bao 1-1. Bao la Yanga lilifungwa na Msuva huku Attram Kwame akiwasawazishia wageni.

Tembo amesifu kiwango cha Msuva na kudai kuwa muda wote alikuwa anajituma uwanjani na kama wangemuacha angefunga mabao mengi.

“Mchezaji aliyevaa jezi namba 27 (Msuva) alitusumbua sana, ana kasi kubwa uwanjani, kama tusingekuwa makini kumdhibiti angetufunga mabao mengi sana, ana kiwango cha juu,” alisema Tembo.

Kuhusiana na matokeo ya sare waliyopata hiyo juzi, Tembo alisema: “Tunashukuru tumetoa sare ugenini, lakini Yanga siyo timu ya kubeza, wana kikosi kizuri, walijipanga kuhakikisha wanashinda lakini wakatoka sare, siyo mbaya itawasaidia mbele.”

Seebait.com 2017

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV