April 5, 2017


Baada ya hivi karibuni timu ya Azam kuchezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga, uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa hauna tena cha kufanya katika michuano ya Ligi Kuu Bara, hivyo vita ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo unaziachia rasmi Simba na Yanga.


Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, aliyasema hayo juzi Jumatatu wakati kikosi cha timu hiyo kilipotembelea makao makuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea jinsi inavyofanya kazi zake, lakini pia kuishukuru kutokana na jitihada zake inazozifanya kwa ajili ya maendeleo ya klabu hiyo kupitia udhamini wake.


Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema kuwa kwa sasa hawana tena nguvu yoyote ya kushindana na Simba na Yanga katika vita ya kuwania ubingwa wa ligi kuu.

“Wakati tunaianza michuano hii lengo letu lilikuwa ni kuwa mabingwa lakini limegonga mwamba kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika baadhi ya mechi zetu.

 “Tumekubali yaishe katika michuano hiyo ya ligi kuu kwani hatuna tena ujanja, hivyo ninachoweza kusema ni kwamba tunazitakia vita njema Simba na Yanga ya kuwania ubingwa huo,” alisema Kawemba na kuongeza:


“Pamoja na hali hiyo iliyotukumba kwenye michuano hiyo ya ligi kuu, matumaini yetu pekee ya kutuwezesha kushiriki michuano ya kimataifa mwakani yamebakia katika Kombe la FA, hivyo tunajipanga kuhakikisha tunalichukua.”

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic