April 19, 2017



Beki mgumu wa Simba, Abdi Banda leo Jumatano atajadiliwa katika Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya sakata lake la kumpiga ngumi kiungo na nahodha wa Kagera Sugar, George Kavila wakati vikosi hivyo vilipopambana Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera ambapo Simba ilifungwa mabao 2-1.


Baada ya kutokea tukio hilo, Banda alishushiwa rungu na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi maarufu kama Kamati ya Saa 72, kwa kusimamishwa kuichezea timu hiyo kwenye michezo yote ya timu hiyo mpaka suala lake lijadiliwe ambapo tayari ameshakosa michezo miwili mpaka sasa ule wa Mbao FC na Toto Africans.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kamati hiyo ndiyo ambayo itakuja na maamuzi juu ya adhabu ambayo itamkuta beki huyo kutokana na kitendo hicho cha kumpiga mwenzake uwanjani tofauti na kanuni za soka.

“Kesho (leo) Jumatano ndiyo suala la Banda litasikilizwa tangu aliposimamishwa na Kamati ya Saa 72, kutokana na kitendo chake cha kumpiga mchezaji wa Kagera Sugar, George Kavila, wakati vikosi hivyo vilipokutana Aprili 2, mwaka huu ambapo ni kinyume na sheria za uendeshaji wa soka hapa nchini.



“Kamati hiyo ndiyo itaamua ni adhabu gani nyingine ambayo anapaswa kupewa beki huyo kutokana na kitendo chake hicho baada ya ile ya kusimamishwa kuichezea timu yake kwenye michezo iliyobakia ambapo mpaka sasa kashakosa mechi mbili,” alisema Alfred.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic