April 15, 2017



Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Celestine ambaye sasa ni katibu mkuu wa TFF, ameitisha kikao cha kamati ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Waehezaji ambacho kinaelezwa kimepewa jina la “komboa pointi za Kagera”.

Taarifa za ndani kutoka TFF zinaeleza, kikao hicho kimepangwa kufanyika Jumanne na kuhakikisha kinarejesha “haki” ya Kagera baada ya Kamati ya Saa 72 kuipa Simba pointi tatu na mabao matatu baada ya Kagera Sugar, kubainika ilimchezesha beki Mohammed Fakhi akiwa na pointi tatu.

“Kweli hicho kikao kimeitishwa na wajumbe wameishatumiwa email, kazi itakuwa ni moja tu kuipa Kagera pointi. Hapa nafikiri wewe hujajua ndugu yangu, Yanga wameungana na kuhakikisha iwe isiwe pointi za Kagera zinarudi. “Baba mwenye nyumba anataka pointi za timu yake zirudi, si unajua ndiye mwenyekiti wa soka Kagera.


“Wakati haya yanatokea, baba mwenye nyumba hakuwepo, alikuwa Morocco. Sasa amerudi na anataka pointi zirudi. Hapa kuna Uyanga, kumbuka viongozi wote wa juu ni Yanga. Lakini usisahau wote wanatokea hukohuko, sasa hizi pointi hata kama Fakhi alikuwa ana kadi tatu, zitarudi,” kilieleza chanzo.



EMAIL YA MWESIGWA KWENDA KWA WAJUMBE:

Kikao cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji
jm selestine <mjselestine@yahoo.co.uk>
To TPLB TPLB <tplb.tplb@yahoo.com>, Boniface Wambura <wambura70@gmail.com>
Cc Jamal Malinzi <jamalmalinzi@gmail.com>, Richard Sinamtwa <richardsinamtwa@gmail.com>
Friday, April 14, 2017 2:06 PM
Click to View Full HTML
Mtendaji Mkuu,
Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).

Hii ni kukufahamisha kuwa kikao cha dharula cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji ya TFF inategemewa kukaa siku ya Jumanne tarehe 18/04/2017 katika hoteli ya Protea Sea View saa 4 asubuhi.Unatakiwa kufika kwenye kikao na wafuatao:
1.Joel Balisidya
2.Rose Msamila
3.Michael Ngogo
3.Match officials wote wa mchezo wa ligi Kuu kati ya Kagera Sugar na African Lyon ie Match comm,centre ref,two assistants na mwamuzi wa nne.
4.Viongozi wa Kagera Sugar

Kila mmoja afike na nyaraka alizo nazo kuhusiana na mchezo huo.TFF itarudisha gharama za safari kwa wale wanaotokea nje ya Dar Es Salaam.

Wasalaam,

Mwesigwa Joas Selestine
General Secretary
Tanzania Football Federation


7 COMMENTS:

  1. Seleh Jembe inaonekana wewe sio Mchambuzi makini.
    Natoa rai kwako,achana na ushabiki wa mpira kàma kama umechagua kazi ya Uandishi

    ReplyDelete
  2. Mmmmh hiyo title inalenga kupotosha na ni hatari sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huu uandishi ni wa kichochezi na tutakushtaki kunakohusika

      Delete
  3. Unapoteza credibility yako uliyojijengea muda mrefu kwa ushabiki wako kwa timu yako ya SIMBA.
    Nasisi tushaacha kununua GAZETI lako unalolisimamia la champion.
    Acha uandishi wa kichochezi

    ReplyDelete
  4. Ukanjanja kwenye nchi hii utaisha lini? Kumbe amewaita walalamikaji na waamuzi kisha akawataka viongoz wa kagera waje na vielelezo ambavyo ni ushahidi wa utetezi wao sasa tatizo lipo wapi? Yeye anataka kuepusha ububusa wa kamati ya masaa 72 baada ya kutoa uamuzi bila ya kuzingatia weledi pale walipoamua kuhukumu kwa ushahidi wa masimulizi ya baadhi ya waamuzi wa mechi hiyo inayodaiwa FAKI alipewa yellow card, wakati walitakiwa watumie ripoti ya waamuzi na si masimulizi yao. Vumilia jamaa kama walivyovumilia wenzio wakiifatilia hii movie wajue mwisho itakuaje

    ReplyDelete
  5. Enter your comment...saleh to taarifa ya kinachotokea usiingize maoni na mtazamo binafsi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic