April 1, 2017
Kikosi cha Simba kesho Jumapili kinashuka uwanjani kupambana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.


Katika kuhakikisha Simba inaibuka na ushindi, Kocha wa Simba, Joseph Omog, ametoa majukumu mazito kwa washambuliaji wake hasa Laudit Mavugo ambayo wanatakiwa kuyafanya ili ushindi upatikane.

Omog amesema majukumu aliyotoa kwa washambuliaji wake hao ni kuhakikisha wanaiongoza timu hiyo kupata mabao ya kutosha katika mchezo huo lakini pia Mavugo kuhakikisha anaiendeleza rekodi yake ya kufunga mfululizo.


Omog  alisema jambo jingine ni kwamba amewataka washambuliaji wake kucheza kwa ushirikiano mkubwa ili wapate mabao.“Hayo ndiyo mambo muhimu ambayo nimewataka washambuliaji wangu kuhakikisha wanayafanya ili tuweze kuibuka na ushindi ili tuweze kujitengenezea mazingira mazuri ya kuibuka mabingwa msimu huu,” alisema Omog.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV