April 8, 2017




MPIRA UMEKWISHAA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Chirwa anajaribu kuwatoka mabeki Alger lakini mwisho unaokolewaDk 87, Kessy anamimina tena krosi safi lakini hakuna mtu pale
Dk 85, Hicham anaruka vizuri lakini Dida anafanya kazi ya ziada kuokoa. Bossou na Cannavaro walitoa nafasi kwa mshambuliaji huyo apige kichwa, ilikuwa hataru kabisa
Dk 84, Ngoma anajaribu tena lakini shuti lake linawababatiza mabeki wa Alger
Dk 81, Chirwa anaachia mkwaju mkali baada ya kuunganisha mpira wa Ngoma, lakini kipa anaudaka vizuri kabisa
Dk 80, wanachofanya sasa Alger ni kuupoza mpira huku wakiwa wamefanya mabadiliko ya kuingiza viungo wote kujiimarisha zaidi katika ulinzi


SUB Dk 79 Emmanuel martin anaingia hapa kwa upande wa Yanga kuongeza nguvu, anachukua nafasi ya Niyonzima
KADI Dk 76 Awadhi Said analambwa kadi ya njano kwa kumvuta Niyonzima hapa
Dk 74 Yanga wanashambulia kama ilivyokuwa awali, lakini bado shida inakuwa umaliziaji. Lakini wanachofanya Alger si kukaa tu nyuma, badala yake wanafanya mashambulizi kadhaa ya kushitukiza
Dk 71, Mwinyi Haji anapata nafasi nzuri, lakini anapiga shuti kuuuuubwaaaa, halina faida
Dk 70, nafasi nyingine nzuri kwa Yanga anaweka kifuani hapa lakini shuti lake chapati kabisa hapa


Dk 68, Alger wanapata kona nyingine baada ya shambulizi. Inachongwa lakini inatua mikononi mwa Dida

Dk 67, Yanga wanaonana sasa, zaidi ya pasi 16 Niyonzima, akigongeana na Kamusoko, Makapu na Kessy lakini krosi inaishia kichwani mwa Chirwa, mpira unatoka juu kidogo
Dk 64, krosi safi ya Kessy, Ngoma anajitishwa hapana, mpira unaangukia kwa Chirwa katika nafasi nzuri lakini anawahiwa hapa
Dk 62, ALger wanaonekana kuamka baada ya kufungwa na wanaanza kushambulia sasa, Govel anaachia mkwaju unaokolewa na kuwa kona
GOOOOOOOOOOOO Dk 60, Kamusoko anaiandikia Yanga bao, baada ya pasi ya Niyonzima kugongeana vizuri na Msuva na kumuachia mfungaji


 Dk 58 sasa, Yanga wanaonekana kuuthibiti mpira vizuri. Lakini bado hawajawa na mipango mizuri katika umaliziaji

Dk 57, Ngoma anajaribu kugeuka lakini kabla ya kupiga mwamuzi anamuambia uliishaotea
SUB: Dk 55 Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Ngoma hapa
Dk 50, krosi nzuri ya Kessy lakini hakuna mtu na Alger wanaokoa
Dk 50 sasa, Yanga wanajitahidi kumiliki mpira vizuri lakini bado inaonekana mipango ya mwisho ni migumu kwao
Dk 48, Cannavaro anamwamgusha Nagesh, amefanya vizuri angemuacha ingekuwa hatari
Dk 45 Yanga wanaanza kwa kasi wakionekana wamepania kuzitumia dakika 45 hizi vizur


MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Chirwa anaingia vizuri tena hapa lakini anadhibitiwa na Nagesh
Dk 43, Kamusoko anatoa pasi nzuri kw aMsuva anaachia shuti lakini inaokolewa na kuwa kona
Dk 40, Alger wanaanza kupoteza mpira kwa kila namna kwa kucheza taratibu
Dk 37, Yanga bado wanajitahidi kuendelea kushambulia lakini hakuna mipango thabiti kuhakikisha wanaipasua mbinu ya Waalgeria
Dk 32, Yanga wanapata kona nyingine baada ya pasi nzuri ya MSuva kuwahiwa na kutolewa. Inachongwa lakini haina faida tena
Dk 31 sasa, Yanga wanaonekana wanataka kufunga bao ili kuwachanganya wapinzani wao na kujiweka vizuri. Lakini mipango mingi inashindikana wanapoingia ndani ya eneo la hatari la Alger
Dk 29, mabeki Yanga wanachanganyana na Mehd anawatoka lakini Dida anafanya vizuri na kuuwahi mpira


Dk 27, krosi nzuri ya Niyonzima, anauwahi Msuva na kumuachia Kamusoko kwa ufundi kabisa, naye anapiga shuti kali na kuokolewa, kona tena kwa Yanga

Dk 25, Niyonzima kwa mara nyingine anaingia vizuri lakini Msuva anaingilia mipango, hawakuwa na mawasiliano
Dk 23, Dida analazimika kufanya kazi ya ziada tena baada ya krosi nzuri ya Hicham
Dk 22, Chirwa akiwa katika nafasi nzuri kabisa anashindwa kufunga hapa, anaukosa mpira
Dk 20, Zidane anaingia vizuri, lakini mwenyewe anashindwa kupiga shuti. Mwinyi haji alimuacha akapita mbele yake
Dk 18, Msuva anaingia vizuri lakini anagongana na Kamusoko hapa


Dk 14, Kamusoko anaingia vizuri lakini mpira anaopiga unamgonga beki wa Alger na kutoka. Ilitakiwa kuwa kona lakini mwamuzi hakuona

Dk 10, Dida anafanya kazi ya ziada kudaka shuti la Goveli ambaye aliingia vizuri na kupiga shuti la chinichini
Dk 8,  kuna mchezaji wa ALger ameumia, anatolewa nje na Yanga wanaendelea kushambulia hapa
Dk 3, Hisham analazimika kutoa mpira akimuwahi Chirwa ambaye aliingia kwa kasi. Unarushwa vizuri lakini unaondolewa tena
Dk 1, mpira umeanza kwa kasi na Yanga ndiyo wanaonekana kushambulia kwa haraka lakini Alger wako makini


KIKOSI CHA YANGA
1. Deogratius Munishi 
2. Hassani Kessy
3. Haji Mwiji
4. Nadir Haroub
5. Vicent Bossou 
6. Juma Saidi 
7. Saimoni Msuva 
8. Thabani Kamusoko 
9. Obrey Chirwa 
10. Haruna Niyonzima 
11. Deusi Kaseke 

Akiba
- Beno Kakolanya 
- Juma Abdul 
- Andrew Chikupe
- Emanuel Martin 
- Geofrey Mwashuiya
- Donald Ngoma

Mfumo : 4-3-3

KOCHA: GEORGE LWANDAMINA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic