Baada ya Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba, kupitia Meneja wa Uwanja Steven Shija kutoa taarifa ya mashabiki wa Simba kuharibu sehemu ya uwanja huo, baadhi ya picha zimewanasa wakiwa katika uharibifu huo.
Mashabiki wa Simba waliharibu uwanja huo kutokana na furaha waliyokuwa nayo baada ya Simba kusawazisha mabao mawili na kufunga la ushindi ndani ya dakika 7 za mchezo.
Shija alisema sherehe za mashabiki hao zilisababisha uharibifu mkubwa kwenye maeneo ya kuingilia wachezaji, waamuzi na geti namba 4, eneo ambalo walikuwa wamekaa mashabiki wa Simba.
Picha zinaonyesha mashabiki hao wakirukaruka juu ya enero hilo la uwanja wakati wakijua si eneo ambalo wanatakiwa kukaa watazamaji.
Mashabiki wa Simba walionekana ni kama waliopagawa mara baada ya Simba kufunga bao la tatu na la ushindi baada ya kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment