April 12, 2017




Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kuanzia kesho Alhamisi Aprili 13, 2017 kwa timu ya Mbeya City itaikaribisha African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.

Kikosi cha Mbeya City kimekuwa kikiandamazwa na sare mfululizo, jambo ambalo kesho kitakuwa kinapambana kuhakikisha kinaepuka sare hizo na kuanza kukusanya pointi tatu.


Jumamosi ya Aprili 15, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Stand United itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga wakati Toto Africans ya Mwanza itaialika Simba SC ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hizi, zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic