April 27, 2017

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amefunguliwa na mashitaka na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB).


TPLB inamtuhumu Mkemi kutoa matamshi ya kuudhi dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mkemi anadaiwa kuwadhalilisha viongozi wa TFF kwa madai kwamba alidai amefikisha suala la viongozi wa kamati ya Saa 72 Takukuru.

Hata hivyo, TFF na bodi ya ligi ziliendelea kukaa kimya bila ya kuchukua hatua hadi wadau walipoanza kulalamika kuhusiana na kufungiwa kwa Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Baada ya hapo, inaonekana ndiyo TFF imekurupuka sasa ikitaka kuona Mkemi naye anachukuliwa natua "ikizuga" kupitia bosi ya ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV