April 6, 2017


Jesse Lingard amesaini mkataba mpya wa miaka minne na Manchester United ambao utamuwezesha kupokea pauni 100,000 kwa wiki kama Man United itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Mkataba huo mpya unamfanya Lingard abaki Old Trafford hadi Juni 2021, huku akipewa nafasi ya kuongeza mwaka zaidi kama atafanya vizuri.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, atakuwa akipokea pauni 75,000 kwa wiki, kama timu yake itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, moja kwa moja mshahara utapanda hadi pauni 100,000 kwa wiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV