April 6, 2017


Bondia Wladimir Klitschko aria wa Ukraine, ameendelea vizuri na mazoezi yake kujiandaa na pambano linalotarajiwa kuwa kali la ngumi za kulipwa dhidi ya Anthony Joshua.


Klitschko ameweka kambi nchini Austria kujiandaa na pambano hilo litakalochezwa Aprili 29 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England.


Hakuwahi kupanda tena ulingoni baada ya kupoteza mikanda yake dhidi ya Mwingereza, Tyson Fury.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 41 anakutana na Joshua mwenye umri wa miaka 27 tu na anayeonekana kuwa ni mahiri na hatari kutokana na anavyochipukia kwa kasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV