April 20, 2017
Timu nne zimetinga nusu fainali ya mabingwa Ulaya. Mbili ambazo ni Real Madrid na Atletico Madrid zinatokea nchini Hispania.

Mbili zilizobaki ni Monaco kutoka Ufaransa na Juventus ya Italia.

Mechi zitakuwa kali na inakuwa vigumu sana kutabiri nani ataingia fainali, lakini Hispania wanaweza kuchagua, “waombe” kukutana wawe na uhakika wa timu ya fainali au kukwepana wajaribu kupeleka mbili fainali. 


Lakini hali inavyoonyesha, zitakuwa ni mechi nne za kukata na shoka kwenda fainali. Je, wewe unampa nani nafasi?

WALIVYOWAHI KUBEBA MAKOMBE YA UBINGWA ULAYA:

TIMU               MAKOMBE
Real Madrid         12
Juventus               2
Monaco                 0
Atletico Madrid     0   

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV