April 20, 2017

BANDA AKIWA TFF AKISUBIRI KUHOJIWA, JANA.
Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji, imefikia uamuzi wa kumfungia beki Abdi Banda, mechi mbili.

Banda amefungiwa mechi mbili baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga ngumi kiungo mkongwe wa Kagera Sugar, George Kavila.

Beki huyo wa Simba anayechipukia, jana aliingia kwenye kikao cha kamati hiyo na kuomba radhi.

Taarifa zinaeleza, Banda aliomba radhi mbele ya kikao baada ya kukiri kosa.

“Kingine kilichomsaidia Banda ni kwa kuwa alimuomba radhi mchezaji husika (Kavila) na mchezaji huyo akakiri kuombwa radhi na Banda,” kilieleza chanzo ndani ya kamati.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV