April 13, 2017
Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 100 katika michuano ya Ulaya.

Bao la 99 na like la 100 amefunga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali wakati Real Madrid ilipoitwanga Bayern Munich kwa mabao 2-1, kwao Munich, Ujerumani.

Amefikisha mabao 100 baada ya kutumia siku 4,264 katika maisha yake ya soka la Ulaya.

Mara ya kwanza kufunga bao la kwanza la Ulaya ilikuwa mwaka 2005, ikiwa katika hatua za kufuzu wakati Manchester United ilipoitwanga Debrecen kwa mabao 3-0.


Tokea mwaka 2005, Ronaldo amecheza jumla ya mechi 140.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV