April 5, 2017

Kikosi cha timu ya taifa chini ya 17, Serengeti Boys leo Jumatano kimesafiri kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kambi maalum kabla ya kuanza michuano ya mataifa Afrika nchini Gabon.

Katika michuano inayotarajia kuanza kutimua vumbi Mei, mwaka huu nchini Gabon, Serengeti imepangwa Kundi B na timu za Mali, Angola na Niger.

Kikosi hicho kimeondoka jioni jijini Dar es Salaam kikiwa na jumla ya wachezaji 20, viongozi sita wa benchi la ufundi na mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana, Ayoub Nyenzi ambapo katika kambi hiyo watacheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kuelekea nchini Gabon tayari kwa mashindano hayo.


 



Kivutio kikubwa ilikuwa ni muonekano wa wachezaji hao ambao walikuwa wamependeza ndani ya mavazi ya suti ambayo yaliwafanya kuwa nadhifu, hata wakati wa upigaji picha walipendeza na kuwa kivutio kwa wasafiri na wasindikizaji waliokuwepo airport hapo.

Ikumbukwe Jumatatu ya wiki hii timu hiyo ilicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ghana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic