April 5, 2017Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema kiwango kilichoonyeshwa na aliyekuwa kipa wao, Juma Kaseja ambaye kwa sasa anaichezea Kagera Sugar, ni cha kawaida na kudai kuwa hajaona cha ziada kwake.


Simba ilipoteza mchezo wake wa Jumapili dhidi ya Kagera Sugar na kujikuta ikiwa nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 55 nyuma ya Yanga yenye pointi 56, huku kipa Kaseja akionekana kuwa kikwazo kutokana na umahiri ambao aliuonyesha uwanjani.


Hans Poppe alifunguka kuwa, kiwango kilichoonyeshwa na Kaseja katika mechi dhidi ya Kagera ni cha kawaida kama alivyokuwa akicheza katika timu yao na kudai kuwa hakuona cha ziada kutoka kwake.

“Ndiyo Kaseja alikuwa mchezaji wetu na aliondoka katika timu yetu miaka kadhaa iliyopita, vilevile amecheza katika timu mbalimbali, kwa upande wangu naona kiwango ambacho amekionyesha katika mechi dhidi ya Kagera ni cha kawaida kama vilevile alivyokuwa akicheza alipokuwa Simba na sijaona cha ziada kutoka kwake, anacheza kama ilivyo kwa makipa wengine.


“Wachezaji wengi wamekuwa wakiondoka na wanaonyesha viwango vya kawaida lakini mwisho wa siku Simba inabakia kuwa ileile,” alisema Hans Poppe.

2 COMMENTS:

 1. Maneno ya mkosaji!
  Hajakosea ni kweli Juma alicheza kiwango cha kawaida na ndicho hicho hicho cha kawaida kilichoikwamisha Simba kupata ushindi!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Alicheza mchezo wa kawaida tu ila simba ni dhaifu sana hawakuweza kumfunga. Hans ni mkweli sana.😀😀

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV