April 28, 2017



Nahodha msaidizi na kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, ametamka kuwa yeye na wachezaji wenzake wote wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri dhidi ya Simba yatakayowapeleka fainali ya Kombe la FA.


Timu hizo, kesho Jumamosi zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Azam iliingia kambini Jumatatu ya wiki hii kwenye makao makuu ya timu hiyo, Azam Complex huko Chamazi, Mbagala, Dar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mao alisema kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya mchezo huo kutokana na maandalizi wanayoendelea kuyapata chini Kocha Aristica Cioaba, raia wa Romania.

“Morali ipo ya wachezaji kwenye timu yetu ipo juu na ninapata matumaini ya ushindi kwenye mechi hii baada ya kurejea kwa wachezaji wetu majeruhi watatu ambao wote ni muhimu kwenye kikosi chetu.

"Kingine ni maandalizi ya timu yetu inayoendelea kuyafanya kwa kuziboresha sehemu zenye upungufu utakaotupa matokeo mazuri,” alisema Mao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic