April 6, 2017


Ingawa ameanza mazoezi ya taratibu lakini Amissi Tambwe amesema ana hamu kubwa ya kuwavaa MC Alger.

Yanga itakutana na MC Alger ya Algeria katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

“Bado sijawa vizuri, naendelea kufanya mazoezi ya taratibu ingawa nikipata nafasi basi nitafurahi,” alisema.

Pamoja na Tambwe kutamani kucheza mechi hiyo. hali yale inaonekana haijaimarika kwa kiwango kikubwa sana.


Hata hivyo, juhudi zimekuwa zikifanyika kuhakikisha Tambwe na Donald Ngoma wanarejea na kuisaidia Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV