April 6, 2017Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Uwanja wa Bunju unaomilikiwa na Simba, Zacharia Hans Poppe amewataka wanachama na mashabiki kujitokeza kuisaidia klabu yao.

Hans Poppe amesema wamefanikiwa kulipa ushuru wa nyasi bandia zilizokuwa zimekwama bandarini.

Lakini akasisitiza: "Sasa kuna suala la uwekaji nyasi pia kuukarabati tena uwanja, hivyo kama wako wanaoweza kuchangia ni jambo jema.

"Niwakumbushe Wanasimba kuwa wanaoweza kuichangia Simba ni wao na si mtu mwingine, hivyo waichangie klabu yao," alisema.

Hivi karibuni kulikuwa na tishio la nyasi hizo kutaka kupigwa mnada na kampuni ya udalali ya Yono kupitia agizo la TRA.

Hata hivyo, Simba iliendelea kusisitiza kuwa kila kitu kilikuwa katika mpangilio na nyasi hizo zisingeuzwa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV