April 1, 2017



Mshambuliaji mwenye kasi, Thomas Ulimwengu anayechezea AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden sasa yupo fiti kwa mapambano baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu.

Ulimwengu alipata majeraha hayo wakati alipokuwa akiichezea TP Mazembe ya DR Congo na hayakuweza kutibika vizuri na alipofika AFC Eskilstuna alijitonesha hivyo uongozi ukalazimika kumpatia matibabu maalumu ya tatizo hilo.

Kutokana na hali hiyo, Ulimwengu alishindwa pia kuja nchini kujiunga na Taifa Stars hivi karibuni kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Botswana na Burundi.

Meneja wa Ulimwengu, Jamal Kisongo, alisema nyota huyo kwa sasa yupo fiti baada ya kupatiwa matibabu maalumu ya tatizo lake lililomsumbua kwa muda mrefu.

“Ulimwengu kwa sasa yupo fiti kabisa ameshamaliza matibabu yake maalumu ya tatizo lake, yupo tayari kwa mapambano.


“Ujue aliumia tangu alipokuwa TP Mazembe lakini hakutibiwa ipasavyo na alipofika Sweden aliumia tena, ndipo ikabidi apatiwe matibabu maalumu ya tatizo hilo.


“Jana (juzi) nimewasiliana naye na ameniambia kuwa anaendelea vizuri na yupo tayari kwa mapambano kuhakikisha anapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza,” alisema Kisongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic