April 18, 2017


Mambo yanaendele baada ya mwamuzi Jonesia Rukyaa kuhojiwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Hii ni ile ishu ya Kagera Sugar, kukata rufaa Simba kupewa pointi tatu na Kamati ya Saa 72.

Baada ya Rukyaa kuhojiwa, sasa wameingia waamuzi wa pembeni, huenda hawa wakawa wa mwisho kabla ya uamuzi kuchukuliwa.

Waamuzi wa pembeni Nicklaus Majaranga na Justin George nao wameingia kuanzia saa 12 na dakika 7 jioni hii.

Kikao hicho kinafanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na uongozi wake umezuia makomandoo wa Yanga na Simba kuingia katika eneo hilo.

Tayari maofisa wa Kagera Sugar pia Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' waliingia kuhojiwa.

Baada ya hapo, kikao hicho kimekuwa kikiendelea na huenda baada ya saa moja au mawili kinaweza kufikia tamati.

Kagera Sugar wamepinga Simba kupewa ponti tatu na mabao matatu kupitia Kamati ya Saa 72 iliyobaini beki Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano.

Tayari imeelezwa majibu yatatolewa leo saa 11, lakini tayari zaidi ya saa moja sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV