April 11, 2017


Unaweza kumekucha kwa kuwa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga imeitaka Bodi ya Ligi Kuu Bara kutothubutu kuwapa pointi tatu za mezani watani wao wa jadi Simba.


Kamati hiyo imekutana jana ikiwa siku chache tangu uongozi wa Simba kumkatia rufaa beki wa Kagera Sugar Mohammed Fakhi ambaye imeelezwa alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo wao uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mjumbe wa Kamati Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi ameiambia SALEHJEMBE kuwa wameliingilia suala hilo lililopo chini ya Kamati ya Masaa 72 ya TFF kwa kuhofia kuwaathiri mbele ya safari wakati wakitetea taji hilo la ubingwa.


Mkemi alisema, tayari wamepeleka malalamiko kwa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na watu wa Cyber ili kuchunguza barua pepe zilizotumwa na mwamuzi wa mchezo huo kwenda kwa Kamati.


"Kamati hii imechelea kutoa maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo dhidi ya Fakhi pia tuna taarifa za kughushiwa email na nyaraka zingine ili kuipa alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe 6 katika kamati hiyo.


"Kama Yanga tumeanza uchunguzi wetu na kutoa taarifa kwa vyombo husika vya dola pia maamuzi yoyote ya kuibeba Simba tutakwenda mahakamani licha ya sheria za FIFA kukataza hivyo kama hawataki tufike huko lazima haki itendeke. 


"Tumeshavijulisha vyombo husika yaani Takukuru, watu wa (cyber crime) na TCRA juu ya uchunguzi wa mawasilano ya waamuzi wote waliosika na kutajwa kwenye rufaa hiyo" alisema Mkemi.

mwisho

1 COMMENTS:

  1. Simba maji yapo puani wanapumulia mipira walivyo dhania sivyo sasa wanatafuta kwa ushindi kwa njia nyengine tunachotaka TFF hizo c mechi zote tatu alizopewa FAKHI hizo kadi za njano watuoneshe video live zote sio kubambanya kwa maneno hayo yametitwa na wakati analogy

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV