April 12, 2017Uongozi wa klabu ya Yanga, umeshindwa kufafanua kwa nini mshambulizi wake, Obrey Chirwa anabaki nchini wakati Yanga inakwenda Algeria kesho kuivaa MC Alger katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema wanaweza kuzungumzia wachezaji walio katika kikosi, si wanaobaki.

“Viongozi ndiyo wanaweza kuzungumzia, lakini ninachojua waliobaki ni majeruhi au wana matatizo ya kifamilia,” alisema.

Uongozi wa Yanga ndiyo haukutaka kutoa ushirikiano kabisa kwa kuwa taarifa zinaelezwa kuwa Chirwa raia wa Zambia, amegoma kwa kuwa anadai mishahara ya miezi mitatu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV