May 28, 2017


Mara baada ya kucheza mechi ambayo Simba imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC na kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho, beki Abdi Band ameaga.

Banda kupitia mtandao wake wa Instagram amewaaga mashabiki wa Simba na kuwashukuru kwa ushirikisho wao.


Beki huyo kinda ambaye katika mechi ya leo aliingia nafasi ya beki wa kushoto baada ya Mohamed Zimbwe Jr kuumia katika dakika ya 47, amesema anakwenda kutafuta maisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV