May 18, 2017




Mshambulizi wa Yanga, Malimi Busungu, amefunguka mambo mawili makuu ambayo ikitokea siku ameondoka ndani ya timu hiyo basi hawezi kuyasahau popote pale aendapo.

Busungu ambaye kwa muda mrefu amepoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho tangu kinanolewa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm kisha Mzambia, George Lwandamina, mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2015/16 akitokea Mgambo JKT, amefanya mahojiano maalum na kipindi cha SPOTI HAUSI kinachorushwa na Global TV Online kila Alhamisi, na kuyataja mambo hayo.

“Kwanza kabisa siku nikiondoka Yanga, kwa yale mazuri sitasahau jinsi mashabiki walivyonipokea wakati najiunga na timu hii, kwa kweli walinipokea vizuri.


“Lakini katika jambo ambalo sipendezwi nalo ndani ya Yanga, ni kitendo cha benchi la ufundi kuamua kumtumia mchezaji mgonjwa na kumuacha mzima nje, kitu hicho huwa hakinifurahishi hata kidogo, imenitokea sana hiyo na nimekuwa mkimya tu kwa sababu siku zote mtu akinikwaza namuacha sitaki na yeye nimkwaze,” alisema Busungu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic