November 18, 2019


Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini amefichua kuwa mikakati yake ni kuona timu hiyo inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika kila msimu.

Mazingiza ambaye amefanya kazi na baadhi ya klabu kubwa za nchini Afrika Kusini ikiwemo Platnumz Stars inayoshiriki ligi ya nchi hiyo maarufu kama PSL akiwa kama meneja mkuu.

Mbali ya Platnumz, Mazingisa ameiongoza Orlando Pirates ‘Buccaneers’ katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2013 huku akizipa mafanikio timu hizo.

Mazingisa alisema kuwa katika mikakati yake ya baadaye aliyonayo ni kutaka kuona Simba inacheza hatua makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa lengo la kuongeza kipato cha timu hiyo.

"Mkakati wangu ni kwamba nataka kuona Simba chini yangu inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kila msimu hilo ndiyo jambo kubwa ambalo naliona kwa sasa.

“Unajua hii michuano kufi ka katika hatua ya makundi inakuwa ni jambo zuri kwa sababu kipato cha timu kinakuwa kinaongezeka, tumepoteza msimu huu ni sawa na kusema ni hasara kwetu lakini tunapoendea nataka kuona kila msimu tunacheza makundi,” alisema Mazingisa.

Ikumbukwe Simba katika msimu uliopita ilifanikiwa kufi ka katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo msimu uliopita ikiwa ni kwa mara ya kwanza kabla ya msimu huu kutolewa kwenye hatua ya awali na UD Songo ya Msumbuji.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic