May 18, 2017


Yanga wameamua kuondoka mapema kabisa kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya mechi yao ya ligi.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, kikosi kizima kinatarajia kuondoka Dar es Salaam kesho kwenda Mwanza kwa ajili ya mechi ya Jumamosi.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema watajua siku ya kuondoka leo baada ya uongozi kulijadili.

"Tuvute subira kidogo kwa kuwa suala hilo kwa sasa lipo kwa uongozi linamaliziwa," alisema leo.

Lakini taarifa nyingine zinaeleza, Yanga wataondoka kesho na ndege kwenda Mwanza na wameona waondoke mapema badala ya kwenda siku moja kabla ya mchezo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV