May 17, 2017



Siku chache baada ya kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kuingia mkataba wa miaka mitano, taarifa zinaeleza sasa mkataba huo utaboreshwa zaidi.


Taarifa za uhakika tokea ndani ya Simba zimeeleza mkataba huo utaboresha kutoka kitita cha Sh milioni 888 kwa mwaka hadi Sh milioni 950.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, awali mkataba walioingia Simba ulikuwa ni Sh bilioni 4.9 kwa miaka mitano lakini sasa mkataba huo utakuwa ni Sh bilioni .

“Ni kweli kabisa, mkataba tulioingia mwanzo sasa umeboreshwa kutoka Sh bilioni 4.9 kwa miaka yote mitano hadi Sh bilioni 5.173,” kilieleza chanzo cha uhakika.

“Unajua wale jamaa wa SportPesa ni waelewa sana, mkataba huu baada ya kuboreshwa utakuwa sawa kwa sawa kabisa na watni wetu Yanga.”

Taarifa zimeeleza kwamba Yanga na SportPesa wanaingia mkataba huo rasmi leo na utakuwa ni sawa kabisa na huo wa Simba baada ya kuboreshwa.

Yanga pia watalipwa Sh bilioni 5.173 kwa mwaka na kufanya timu hizo ziwe zinalipwa sawa kila kitu.

Hivi karibuni baada ya Simba kusaini mkataba mpya kulizuka tafrani hadi Zacharia Hans Poppe akatangaza kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji na uenyekiti wa kamati ya usajili.

Hata hivyo, baadaye Hans Poppe alizungumza na viongozi wa Simba waliomuomba arejee tena.

Kumekuwa na taarifa viongozi hao pia kuzungumza na Mohamed Dewji ambaye pia aliamua kujiweka kando akiwa na madai sawa na yake ya Hans Poppe, kutoshirikishwa.


1 COMMENTS:

  1. :-) hawa matopeni wanachekesha, eti na sisi tunataka kama watani zetu dah! Maendeleo kisoka bongo sidhani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic