May 27, 2017



GOOOOOOOOOO  Dk 120 Kichuya anaifungia Simba bao la pili
 PEAAAAAAAT Dk 109, Simba wanapata penalti baada ya beki kushika shuti la Juuko
DK 105, Blagnon anaachia shuti kali hapa lakini linapiga nyavu za nje na mashabiki wanadhani ni bao
GOOOOOOOOO Dk 109 Ndaki Robert ambaye mabeki wa Simba waliamini ameotea anaandika basi safi kabisa kwa Mbao FC hapa
Dk 106, Kotecha tena anaachia mkwaju hapa lakini goal kick
Dk 105 Kotecha anaingia vizuri kabisa hapa lakini goal kick


MAPUMZIKO
Dk 104 Ndikumana anajichanganya na kipa wake, inakuwa konaaa
SUB Dk 104 Ndaki Robert anaingia na Rajesh Biku Kotecha upande wa Mbao
Dk 103, Banda anaachia mkwaju mkali hapa lakini juuuuu
Dk 100 sasa, mpira umekuwa butuabutua, presha inaonekana kuwa kubwa na kila upande unapoteza utulivu
Dk 98, Agyei anaruka vizuri na kudaka mpira wa krosi wa Ambundo, ilikuwa hatari


GOOOOOOOOOOOOOOO Dk 95, Blagnon anapokea mpira wa Banda na kuachia mkwaju mkali kabisa hapa na kuandika bao la kwanza kwa Simba
Dk 94 Mavugo katika nafasi nzuri lakini hakulenga lango
DK 92, Mavugo anapiga shuti la hooovyooooo, goal kick
Dk 91, Habib anaachia mkwaju mkali langoni mwa Simba, lakini hakulenga. Goal kick

MWISHO WA DAKIKA 90 (SUBIRI DAKIKA 30 ZA NYONGEZA)
-Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini kipa anaokoa kwa ustadi mkubwa kabisa

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 zimekamilika, Simba wanashambulia zaidi na Mbao kiana wanapoteza uda huku wakivizia nafasi, wafanye yao
Dk 86, Simba wanapata mpira wa faulo lakii  Kichuya anafanya kituko
Dk 84 Kipa Haule anaokoa mpira kwenye mwamba anaokoa kichwa cha Juuko na kuwa kona, inachongwa anaokoa tena
Dk 83 Simba wanapata kona, Mkude anaachia mkwaju, kona tena


Dk 82, mabeki wa Simba wanajichanganya hapa lakini Bukungu anakuwa makini, anaotoa
Dk 80 Mwamuzi anakwenda kumuasa kipa Haule kwa kupoteza muda akidai anafunga viatu
SUB Dk 80 Ndemla anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Frederic Blagnon
Dk 80, Ajibu anafanya vema lakini Ndemla anaonekana kutokuwa makini mara kadhaa
Dk 74, Mavugo anashindwa kuunganisha krosi safi ya Ajibu na mpira unakwenda nje na kuwa goal kick
DK 71, Mkwaju safi wa adhabu wa Ndikumana lakini Agyei anaonyesha umahiri kwa kudaka vizuri kabisa hapa
KADI Dk 70, Mkude analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Hoza, ni eneo zuri kwa Mbao


Dk 69 Maganga anawachambua mabeki anawachambua mabeki wa Simba hapa lakini Juuko anatoa na kuwa kona
Dk 65, kipa Haule yuko chini baada ya kugongana na beki wake wakati akimuwahi Juuko asipige kichwa mpira wa adhabu wa Ajibu
Dk 63, shuti jingine kali langoni mwa Mbao, safai hii ni Ndemla lakini goal kick
Dk 63 Banda anaachia shuti jingine, lakini nyanya kabisa kwa Haule
Dk 61 Bukungu analazimika kulala tena chini na kutoa nje, kona. Inachongwa, Simba wanaokoa
SUB Dk 60, Liuzio anakwenda benchi na bwana harusi, Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi yake
Dk 60, Banda anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini goal kick


SUB 59 Dickson Ambundo anaingia kuchukua nafasi ya Sangija upande wa Mbao FC
KADI Dk 57, Asante analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mavugo
Dk 57, nafasi nzuri ya kwanza ya Mbao katika kipindi cha pili baada ya Mkude kuanguka lakini Mbao wanapoteza
Dk 55, nafasi nyingine ya Simba lakini krosi ya Kichuya, mavugo anashindwa kuuwahi mpira
SUB Dk 51 Zimbwe anakwenda nje baada ya kuumia, nafasi yake ianchukuliwa na Abdi Banda
Dk 50, Simba wanagongeana vizuri karibu na lango la Mbao, lakini mara nyingine wanapoteza utulivu
Dk 48, shuti kali la Kichuya linampita kipa lakini Ndikumana anaokoa ukiwa unajaa wavuni. Kona inachongwa lakini haina faida
Dk 45, kipindi cha pili kimeanza kwa kasi kwelikweli, kila timu inaonekana imepania kufunga bao la mapema


MAPUMZIKODAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45, krosi safi ya Kichuya kwa mpira wa adhabu, Asante anaokoa hapa
KADI Dk 44, kadi ya kwanza ya njano ya mchezo inakwenda kwa Swita ambaye anamuangusha Zimbwe Jr aliyekuwa akichanja mbuga
Dk 40, Muzamiru anaachia mkwaju mkali akiwa nje, goal kick


Dk 38 mpira unaonekana kuwa umepoa sana, ingawa Simba ndiyo wenye mashambulizi mengi lakini hawana utulivu wakifika kwenye lango la Mbao
Dk 33 Mavugo anamdhibiti Asante na kuachia mkwaju mkali hapa, kona
Dk 32, nafasi kwa Kichuya lakini anabutua buuuu
Dk 29, Simba inapata kona ya pili baada ya kipa Haule kujichanganya, inachongwa lakini haule anadaka vizuri kabisa
Dk 27 kosa kubwa wanafanya Mbao FC, Mavugo anapewa pasi yeye na kipa, alichofanya, anakijua mwenyewe, goal kick


Dk 26, Mavugo anauwahi mpira lakini anamgonga kipa hapa na Mwamuzi wa mchezo wa Kikumbo anasema faulo
Dk 22 Simba wanafanya shambulizi hapa, Mavugo anapiga inazuiwa, Liuzio anapiga inazuiwa na Mbao wanaondosha
Dk 20 sasa, bado mpira haujatulia sana na mpira bado hauna mipango mingi madhubuti kwenye milango
Dk 15, Mbao FC wanapata kona ya kwanza pia baada ya mpira kumgonga Zimbe Jr, inachongwa lakini Mavugo anaokoa hapa
Dk 14, Kipa Haule wa Mbao anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kona wa Kichuya
Dk 13, Simba wanaingia vizuri hapa, Kichuya anakwenda lakini mwambeleko anatoa na kuwa kona ya kwanza
Dk 12, Bukungu anajaribu shuti kali umbali wa mita 50, lakini goal kick


Dk 10, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa baada ya kubaki karibu na lango la shuti lake linatoka juuu
Dk 7, mpira wa adhabu, Mavugo anajaribu kuachia shuti lakini Kwassi Asante anawahi na kuokoa
Dk 4 shuti kali, Agyei anatema lakini Swita karibu kabisa na lango anapaisha
Dk 3 Kipa Mbao FC anatoka na kuuwahi mpira mbele ya Mavugo hapa
Dk 3 Mohamed Zimbwe anajichanganya hapa lakini kipa anafanya kazi ya kuokoa kwa miguu
Dk 1, mpira umeanza, Mavugo anaubutua nje kule na Simba wanasogea karibu na lango la Mbao FC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic