May 21, 2017


FULL TIME
Mchezo umemalizika.
 
Dakika ya 94: Mchezo unaelekea kumalizika. Kipa wa Niger anapatiwa matibabu, baada ya kuinuka mwamuzi anampa kadi ya njano kw akupoteza muda.

Dakika ya 90: Zinaongezwa dakika 4.

Dakika ya 88:  Serengeti wanapata mpira wa kurusha, unarushwa ndani ya eneo la 18 la Niger lakini beki wao anaubutua na kuokoa.

Dakika ya 81: Presha inazidi kuongezeka kwa Serengeti kutokana na kuwa nyuma kwa bao moja.

Dakika ya 76: Mchezo unaendelea kwa kasi, presha kubwa ipo kwa Serengeti kutafuta bao la kusawazisha.

Dakika ya 70: Mashambulizi sasa yamehamia upande wa Niger.

Dakika ya 64: Mchezo unandelea, Serengeti wanapambana kutengeneza mashambulizi.

Dakika ya 61: Kipa wa Niger anaumia mikononi wakati akiwania mpira kwenye kuokoa shambulizi. 

Dakika ya 55: Niger wanafika langoni mwa Serengeti lakini mpira wa kichwa unapaa juu ya lango.

Dakika ya 51: Serengeti wanapata nafasi ya wazi lakini wanashindwa kutumia nafasi.

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

Kipindi cha kwanza kimekamilika.

Dakika ya 45: Inaongezwa dakika 1.

Dakika ya 42: Niger wanapata bao kwa kichwa, mfungaji ni Ibrahim. Aliunganisha mpira wa kona.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 41: Mchezo baso unaendelea kwa kasi.

Dakika ya 37: Nafasi ya wazi inapatikana kwa Serengeti wanashindwa kuitumia, straika alibaki yeye na kipa akapiga shuti likaoka nje.

Dakika ya 35: Niger wanaendelea kutafuta bao kwa nguvu kwa kuwa wanajua sare itawaondoa mashindanoni.

Dakika ya 30: Mchezo unaendelea kuwa wa kushambuliana kwa zamu baina ya timu zote.

Dakika ya 20: Niger wanaokoa mpira wa kona langoni kwao, kisha wanakimbia na mpira kufanya shambulizi kali lakini kipa wa Serengeti anapangua kisha anaudaka tena mpira.

Dakika ya 18: Niger wanafanya shambulizi kali lakini inapuliwa filimbi kutokana na mchezaji woa mmoja kucheza faulo.

Dakika ya 16: Serengeti wanatengeneza nafasi lakini inapulizwa filimbi ya kuotea.

Dakika ya 12: Niger ambao wanaonekana kuwa warefu wanapata kona mbili lakini wanashindwa kuzitumia vizuri.

Dakika ya 10: Niger wanafika kwenye lango la Serengeti lakini kazi nzuri ya walinzi wa Serengeti inafanya kazi.

Dakika ya 5: Mchezo bado hauna kasi kubwa.

Dakika ya 2: Timu zinaanza kusomana taratibu.

Mchezo umeanza.

Waamuzi wanazungumza na manahodha. Huu ni mchezo wa Kundi B wa michuano ya Afrika kwa Vijana (Afcon) kwa mwaka 2017 nchini Gabon.

Timu zinaimba nyimbo za taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic