May 21, 2017




Serengeti Boys inayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika sasa uhakika itamkosa nahodha wake baada ya kurejeshwa nchini.

Nahodha Issa Abdi Makamba, amerejeshwa nchini kutoka Gabon baada ya kuvunjika kidole.

Makamba alikwenda Gabon na wenzake kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo inayofanyika nchini humo, siku tatu kabla ya kuanzia kwa michuano hiyo alivunjika kidole cha mguu wa kulia na kumfanya aondolewe kwenye mipango ya kikosi hicho.

Licha ya kuonekana hawezi tena kushiriki michuano hiyo, Makamba aliendelea kubaki kambini na wenzake kwa takribani wiki moja kabla ya kurudishwa nchini jana.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema: “Kuna sababu kuu mbili zilizofanya mpaka Makamba akarudishwa Tanzania, kwanza ni kitendo cha Caf (Shirikisho la Soka Afrika) kutusafirisha kutoka mji mmoja kwenda mwingine kwa ajili ya mchezo wetu wa mwisho wa makund.

“Hivyo kwa hali yake haipaswi asafiri kwa kuwa itakuwa kama kumsumbua.

“Sababu nyingine ni kwamba anapoendelea kubaki na wenzake na kuhudhuria mechi akiwa jukwaani inazidi kumuumiza zaidi sababu anatamani na yeye angekua anacheza, hivyo madaktari wameshauri arudishwe tu nyumbani.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic