May 5, 2017

Manchester City wameingia kwenye anga za rungu la FA ya England baada ya kufungiwa kusajili wachezaji vijana chino ya miaka 18.

Man City imefungiwa kusajili wachezaji wa aina hiyo kwa miaka miwili ikiwa ni pamoja na kupigwa faini ya pauni 300,000 baada ya kubainika walivunja sheria za usajili.


Imeibainika kwamba walivunja kanuni za Premier League baada ya kujaribu kumsainisha mchezaji ambaye alikuwa na mkataba na timu nyingine bila ya kufuata utaratibu sahihi.

Inaonekana Man City walifanya mazungumzo na familia ya kijana wakati akiwa bado na mkataba na klabu nyingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV