May 14, 2017


Picha zimesambazwa mitandaoni zikimuonyesha mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu akidaiwa kuwa amelewa chakari.

Busungu anaonekana akiwa katika usingizi mkali huku pembeni yake kukiwa na chupa.

Moja ya kundi linaloundwa na mashabiki wa Yanga la “Naipenda Yanga”, limetupia picha hizo mtandaoni likibainisha Busungu yuko chakari mchana huu katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.


Juhudi za kumpata Busungu ambaye amekuwa nje ya kikosi hizo zimekuwa ngumu kutokana na simu yake kuendelea kuita.

Awali ilielezwa, Busungu aliondolewa katika kikosi cha Yanga baada ya kususa baada ya kufanyiwa mabadiliko na Kocha George Lwandamina.

Mara kadhaa, amekuwa akilalamika kutokana na kutopewa nafasi wakati wa Kocha Hans van der Pluijm aliyemsajili kutoka Mgambo Shooting ya Tanga.

Hata hivyo, kwa upande wa Lwandamina ambaye alichukua nafasi ya Pluijm, inaonekana pia hajafurahishwa na suala lake la kususa, hivyo amemuacha akae nje ya kikosi.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV