May 14, 2017



Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuandika barua yake kuachia ngazi kwenye kamati ya utendaji.

Maana yake, moja kwa moja Hans Poppe anaondoka kwenye kamati ya usajili.

Akizungumza katika mahojiano maalum na SALEHJEMBE, Hans Poppe amesema hakuridhishwa na namna viongozi wa juu wa klabu hiyo walivyoshiriki katika mchakato wa mkataba na kampuni ya ubashiri na SportPesa.

“Nimeamua kuondoka, utaona mambo hayakuwa sawa. Kulikuwa na siri na uficho na hata ushiriki wa kamati ya utendaji haukuwa sawa.

“Waliamua kufanya mambo kwa uficho na hadi wanasaini mkataba hakukuwa na uwazi wa mambo. Sitaki kuwa sehemu ya maamuzi ambayo yanakiuka uungwana,” alisema.

Simba imeingia mkataba wa Sh bilioni 4.9 ambao utadumu kwa miaka mitano.
“Napenda kuwa wazi, sikufurahishwa na mambo yalivyokwenda. Inaonekana kama kuna vitu vya pembeni jambo ambalo siwezi kukubaliana nalo.”


Hans Poppe amekuwa moja ya nguzo ya Simba wakati wa shida, pia katika usajili wa klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic