May 18, 2017Beki Method Mwanjale sasa yuko fiti na anaweza kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Simba.

Mwanjale amekuwa majeruhi kwa zaidi ya miezi miwili, Simba ikihangaika katika safu ya ulinzi iliyoonekana kupwaya.

Simba tayari ipo kambini Dege Beach nje kidogo ya jijini La Dar es Salaam ikijiandaa na mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC.

Mbali na Mwanajale, mchezaji mwingine ambaye yuko fiti ni Jamal Mnyate ambaye pia amekuwa akifanya mazoezi na wenzake na sasa yuko fiti.

Katika mechi za mwisho, Simba ilionekana kuathirika na kuandamwa kwa majeruhi mfululizo.


Mwanjale alionekana kuwa kisiki katika ulinzi hasa katika mechi za kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV