May 18, 2017
Simba wanataka kushinda mechi ya mwisho dhidi ya MWadui FC bila kujali chochote kitakachotokea.

Ukitaka kupata uhakika wa hilo, utaona hivi, Simba wameamua kuchukua wachezaji wao wote na kwenda nao kambini.

Simba imeweka kambo Dege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mechi hiyo.

“Kweli ni kikosi chote kipo hapa kambini, tunajiandaa na mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC,” alisema Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’.


Kabla Simba wamekuwa wakiingia kambini na wachezaji baadhi huku wengine wakiwa nje ya kambi hasa wale ambao wanakuwa hawatarajii kucheza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV