May 30, 2017Nahodha wa Mbao FC, Yusuf Ndikumana amesema wameamua kuacha kila kilichotokea katika fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba na kuangalia nini wafanye kwa ajili ya msimu ujao.


Simba iliishinda Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Shirikisho. Lakini Mbao FC walilalamika kuwa bao la pili lililotokana na penalti ya Shiza Kichuya, lilikuwa na walakini.

Ndimkumana amesema wanaangalia wafanye nini kwa ajili ya msimu ujao ambalo ni jambo muhimu zaidi.

“Tutafanyaje, hatuwezi tena kurudisha jambo katika kipindi hiki, tunachofanya ni kuangalia cha kufanya msimu ujao,” alisema.


Awali, Ndikumana alifanya kazi ya ziada katika mchezo huo kuwazuia wachezaji wa Mbao FC wasimvamie mwamuzi wakati wakipinga penalti hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV