Kikosi cha Ruvu Shooting kimepata ajali kikiwa njiani kurejea Pwani kutoka Shinyanga ambako walimaliza mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United.
Wachezaji watatu pamoja na Msemaji wa Shooting, Masau Bwire ndiye wamepata majeraha madogo.
Masau Bwire amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Manyoni, saa 3 asubuhi baada ya tairi la gari hilo upande wa kushoto kupasuka na gari kuingia porini.
“Baada ya tairi kupasuka tumeingia porini kama mita mia nne hivi gari likipiga visiki, mawe lakini dereva kajitahidi.
“Tunamshukuru Mungu majeraha si makubwa sana, pia daktari wetu mwanamama amefanya kazi nzuri.
“Pia wachezaji watatu Hamisi kisuke, Abdul Mpandika aliyeumia mguu na Said Dilunga. Lakini sote tunaendelea vizuri,” alisema Masau Bwire.
Wachezaji hao wataendelea na safari hapo baadaye sasa wanasubiri gari jingine kutoka Dodoma ambalo linakwenda kuwachukua ili waendelee na safari.
SALEHJEMBE INATOA POLE KWA WANARUVU SHOOTING NA KUWAOMBEA WALIOPATA MAJERAHA WAPONE HARAKA.
0 COMMENTS:
Post a Comment