May 24, 2017
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo imezindua ligi itakayojulikana kama SportPesa Super Cup.

Ligi hiyo itashirikisha timu nne kutoka Tanzania na Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa na mshindi wa pili.


Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema ligi hiyo inatarajiwa kuanza  Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11.

“Utakuwa ni ushindani wa timu nne, kutoka Tanzania na Kenya. Hawa ni majirani na siku zote ni wapinzani wakubwa,” alisema.


Bingwa wa SportPesa Super Cup ataondoka na kitita cha dola 30,000 huku mshindi wa pili akipata dola 10,000.

SportPesa ndiyo wadhamini wapya wa timu tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni rekodi mpya.

Tayari wameidhamini Simba kwa mkataba wa miaka mitano, halafu wakafanya hivyo kwa wakongwe wengine Yanga kabla ya kuidhamini Singida United ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV