May 24, 2017



Baada ya timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys kutolewa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana, wachezaji wa timu hiyo wamewaomba radhi Watanzania kutokana na matokeo hayo.

Jumapili iliyopita, timu hiyo ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Niger ukiwa ni mchezo wa mwisho wa Kundi B ambapo matokeo hayo yameifanya Serengeti Boys kumaliza nafasi ya tatu na pointi nne hali iliyosababisha kutupwa nje ya michuano hiyo.

Kutokana na kuondoshwa huko, kikosi hicho kinatarajiwa kurejea nchini kesho Alhamisi kutoka Gabon ambako michuano hiyo ya vijana inafanyika.

Mwenyekiti wa Maendeleo ya Soka la Vijana Tanzania, Ayubu Nyenzi, amesema: “Tangu vijana watolewe katika mashindano, wamekuwa hawana raha na wanawaomba Watanzania wawasamehe kwa matokeo hayo mabaya.


“Tunatarajia kurejea Tanzania Alhamisi, tumejifunza mengi katika michuano hii hali ambayo inatufanya tujipange na kutorudia makosa kwenye michuano kama hii itakayofanyika mwaka 2019 ambapo sisi tutakuwa wenyeji.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic