May 20, 2017


Na Mwandishi Wetu, Mwanza
 Tiketi kati ya mechi yan mwisho ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba zimezua tafrani kubwa jijini hapa.


Tafrani limezuka baada ya kuwasili kwa tiketi hizo na kila shabiki akitaka kupata ili awahi kuingia uwanjani.

Kwenye Uwanja wa Nyamagana, watu walikuwa wakikata tiketi na kusababisha vurugu kubwa hadi askari walipoingilia na kutuliza.

Tiketi hizo zimechelewa kufika jijini Mwanza ikielezwa aliyekuwa akizileta alipata dharura.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV