September 28, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kipo njiani hivi sasa kurejea Dar es Salaam kukamilisha maandalizi ya mwisho dhidi yake na Simba baada ya kukamilisha kambi mjini Morogoro.

Yanga itakuwa mgeni dhidi ya Simba Septemba 30 2018 ambayo ni Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga inaenda kucheza mchezo huo ikiwa imeshinda mechi zake nne mfululizo za msimu huu huku Simba ikishinda mbili, sare moja na ikifungwa moja.

Aidha, Simba watakuwa wanacheza na Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi ya mwisho waliyokutana Aprili 29 2018 kwa bao 1-0.

Tayari mashabiki wanazi wa timu hizo mbili wameshaanza tambo kuelekea mechi hiyo yenye msisimko wa aina yake ambapo kila mmoja akiamini atapata matokeo.

5 COMMENTS:

  1. Simba imeshinda mechi tatu na sio mbili.Memory ya mwandishi mbovu au unazi?

    ReplyDelete
  2. daaah hii mechi ipite tu,si kwa kuendelea kutuchanganya na habri zenu hizi

    ReplyDelete
  3. Kweli Maana hata anaoandika hawajui anaandika nn simba kashinda mechi tatu siombili

    ReplyDelete
  4. Kweli Maana hata anaoandika hawajui anaandika nn simba kashinda mechi tatu siombili

    ReplyDelete
  5. Kwani Yanga anakuja kuimaliza Simba alishaanza kucheza ndugu mwandishi? Naona kama habari yako imeegemea upande mmoja sana. Yanga anakuja kupambana na Simba kwenye mchezo wa kwanza kwa mwaka huu mpya wa ligi soka Tanzania Bara.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic