February 5, 2020


KIKOSI cha Yanga leo kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Lipuli FC ya Iringa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Balama Mapinduzi dakika ya 14 akimalizia pasi ya Juma Abdul na lile la pili lilifungwa na Bernard Morrison dakika ya 32 akimalizia pasi ya Abdul.

Bao pekee la kufutia machozi kwa Lipuli lilifungwa na David Mwasa dakika ya 58 kwa mpira wa adhabu uliozama jumla kimiani.

Huu unakuwa ushindi wa tatu mfululizo kwa Yanga iliyo chini ya Luc Eymael kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, ilianza kushinda mbele ya Singida United mabao 3-1 , mbele ya Mtibwa Sugar ilishinda bao 1-0 na leo imeshinda mabao 2-1 mbele ya Lipuli FC.

5 COMMENTS:

  1. Hata tukikosa ubingwa lakini tunacheza kiuhalali kabisa

    ReplyDelete
  2. Samahani wana simba haina haja yakuchukua nafasi kuanza kulalama kama wenzetu,nadhan kwa macho yetu tumejionea hivyo tunawaomba muonyeshe utofauti kwamba nyinyi ni watu mnaojielewa NYAMAZAENI KIMYAA TUONE WATATULETEA VAR YA GOLI LILIOKATALIWA??.

    ReplyDelete
  3. Na mtuletee na goli alilofungwa azam na prizon pia mlikatae maana nyinyi mmeshakua lialia footbal club,mnashindwa kupambana na hali yenu mnatafuta sababu ili mpate kisingizio,mpira ndivyo ulivyo je na nyie mmependelewa??kwahiyo mlinunua mechi maana sheria inasema lile ni goli la halali kabisa,msiwe mnaongea mpaka mnapitiliza waungwana.

    ReplyDelete
  4. Ongelea pia lile goli alilofunga Amisi Tambwe Simba kabla ya dhahiri kuunawa mpira na kukubalika

    ReplyDelete
  5. Mie nawashangaa wanasimba wenzangu hivi Kwa nini upoteze muda wako kubishana na hawa vyura wanaolialia kila kukicha?kumbukeni kelele za vyura hazimzuii mnyama kunywa maji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic