May 16, 2017Wakati inaonekana itakuwa ni kazi rahisi kwa Yanga kubeba ubingwa hii leo kwa kuifunga Toto African ya Mwanza, wao wanafikiria tofauti kabisa.

Yanga inashuka dimbani Taifa jijini Dar es Salaam, kucheza na Toto African ya Mwanza. Kama itashinda, basi itafanikiwa kutetea ubingwa wake.

Toto African wanaamini mambo hayatakuwa rahisi kama Yanga wanavyodhani kwa kuwa wanajua wakifaya hivyo, basi safari yao imefikia mwishoni.

Msemaji wa Toto, Cuthbert Japhet anasema wamejiandaa na wanazitaka pointi tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuepuka kuteremka.

“Mechi na mabingwa watetezi haiwezi kuwa rahisi, tunataka kufanya vizuri na tumejiandaa kucheza kwa nidhamu na ushindani,” alisema.


Yanga wanachotaka ni kubeba ubingwa na si zaidi kwa kuwa wanajua mechi yao dhidi ya Mbao FC huenda ikawa ngumu zaidi kama watashindwa kufanya vizuri leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV