May 16, 2017


Kikosi cha Hull City kimeporomoka kutoka Ligi Kuu England. Lakini wadhamini wake, kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, imeendelea kubaki kwenye Ligi Kuu England.

SportPesa wataendelea kubaki kwenye Ligi Kuu England baada ya kutangaza udhamini na Everton, moja ya timu kubwa za ligi hiyo.


Udhamini huo ulitangazwa jana na kuifanya SportPesa kuwa wadhamini wapya watakaoonekana kwenye vifua vya wachezaji na mashabiki wa Everton kuanzia msimu ujao kwa kuwa mkataba huo unaanza Juni Mosi, mwaka huu.

Kwa hapa Tanzania, tayari SportPesa ni wadhamini wa Simba SC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV