May 16, 2017Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva hatafunga tena mabao, maana yake atabaki na mabao yake 14.

Hii inatokana na Msuva kuumia katika mechi dhidi ya Mbeya City mara tu baada ya kufunga bao lake la 14 na sasa ndiyo anaongoza.

Taarifa zinasema Msuva atalazimika kuzikosa mechi mbili zilizobaki za Ligi Kuu Bara, dhidi ya Toto African leo pia dhidi ya Mbao FC.

Kwa Msuva atakuwa akiomba dua washambulizi wengine Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting mwenye mabao 13, Mbaraka Yusuf wa Kagera mwenye 12 kama Obrey Chirwa wasifunge na kumfikia au kumpita.LISTI:
Simon Msuva              14
Abdulrahman Mussa   13
Mbaraka Yusuf            12
Obrey Chirwa              12
Shiza Kichuya             11

Amissi Tambwe           10

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV