May 16, 2017


MPIRA UMEKWISHAAAAA
-SUB Justine Zulu anaingia zikiwa zimebaki sekunde 30 tu, anachukua nafasi ya Haruna Niyonzoima

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Toto wanaonekana wamepania kusawazisha na wanapiga mipira ya juu kwenye lango la Yanga ili wajaribu bahati yao

KADI Dk 88, Carlos Protas analambwa kadi ya njano baada ya kumkata ngwala Juma Abdul
Dk 88, Juma Abdul yuko chini bado akigangwa ni baada ya kupiga krosi akaanguka
Dk 87, Malima analazimika kutoa nje krosi kali ya Juma Abdul

Dk 86, Kaseja anaachia Mkwaju mkali baada ya Martin kuambaa na mpira na Chirwa kutoa krosi safi kabisa
GOOOOOOOOO Dk 81, krosi safi ya Juma Abdul, Tambwe anaruka na kupiga kichwa safi kinachotinga wavuni kama roketi
Dakika 80, kipa Kisu anafanya kazi nyingine ya ziada kuokoa mpira wa kichwa wa Tambwe

Dakika 79 kipa Kisu anapangua mpira wa kichwa ambao ulikuwa unajaa wavuni
Dakika 78, mpira ulikuwa umesimama kwa takribani dakika mbili baada ya mchezaji mmoja wa Toto kuumia
Dk 75 nafasi nyingine nzuri kwa Yanga lakini Chirwa anashindwa kufunga
Dakika  74 Mwinyi Haji anaachia mkwaju mkali kabisa lakini juuu

Sub Dakika 71 Mwashiuya anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dakika ya 70: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoa Mwashiuya, anaingia Emmanuel Martine.
  
Dakika ya 65: Timu zote zinaendelea kushambuliana kwa zamu.

Dakika ya 60: Yanga wanaelekea langoni mwa Toto, wanapata kona, inapigwa lakini inakuwa haina faida.

Dakika ya 58: Waziri Jr wa Toto anaingia na mpira, anatoa pasi lakini wenzake wanashindwa kuitumia vizuri.

Dakika ya 55: Natoka Mohamed Soud wa Toto, anaingia Waziri Ramadhan.

Dakika ya 50: Kaseke ameongeza uhai kwenye safu ya kiungo ya Yanga.

Dakika ya 48: Lusajo anamchezea faulo Bossou, inakuwa faulo kueleka kwa Toto.

Dakika ya 45: Yanga wameanza kwa kasi.

Kipindi cha pili kimeanza.

Yanga wanamtoa Juma Mahadhi, nafasi yake inachukuliwa na Deus Kaseke.

Timu ndiyo zinarejea kwa ajili ya kipindi cha pili.




MAPUMZIKO

Dakika ya 48: Mwamuzi anapuliza filimbi kumaliza kipindi cha kwanza.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 44: Juma Mahadhi anaingia na mpira lakini anakosea, Kamusoko anauwahi mpira, Yanga wanacheza pasi ndefu.

Dakika ya 42: Kamusoko anawatoka walinzi wa Toto, anapiga shuti lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 40: Chirwa anaingia na mpira lakini beki wa Toto anamzuia na kuutoa mpira inakuwa kona.

Dakika 37: Yanga wanafanya shambulizi kali, Thaban Kamusoko anapiga shuti kali kipa analipangua inakuwa kona lakini wanashindwa kufanya kazi nzuri ya kumalizia kazi waliyoianza.

Dakika ya 34: Juma Abdul wa Yanga anaumia na mchezo unasimama kwa muda apatiwe matibabu.

Dakika ya 32: Yanga wanajibu mashambulizi, wanalishambulia lango ya Toto, wanamiliki mipira.

Dakika ya 28: Toto wanaanza kujipanga vizuri na kuonyesha kuelewano, wanafanya mashambulizi katika lango la Yanga, wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.

Dakika 25: Toto wanapata nafasi ya kushambulia lakini nahodha wao Lusajo anashindwa kuitumia nafasi anayopata, mpira unaokolewa.

Dakika ya 20: Kasi ya Yanga imepungua tofauti na walivyoanza lakini wanaendelea kufika langoni mwa Toto mara kadhaa.

Dakika ya 15: Chirwa anaonyesha kuwa mpambanaji, Yanga wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.

Dakika ya 10: Chirwa anachezewa faulo.

Dakika ya 5: Toto wanarudi nyuma wachezaji wao kuanza kuzuia.

Dakika ya 2: Yanga wanaendeleza kasi kama kawaida, inavyoonekana wanatafuta bao la mapema.

Dakika ya 1: Yanga waanza kwa kasi
Mwamuzi anaanzisha mchezo


Kikosi cha Yanga ambacho kitashuka uwanjani leo kukipiga dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika Ligi Kuu ya Vodacom tayari kimeshatoka, wachezaji 11 watakaoanza hawa hapa:
1. Beno Kakolanya
2. Juma Abdul,
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vincent Bossou
6. Thaban Kamusoko
7. Juma Mahadhi
8. Haruna Niyonzima
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Geofrey Mwashuiya
Akiba
Deogratius Munishi, Hassan Kessy Nadir Haroub, Matheo Antony, Deusi Kaseke , Emmanuel Martin na Justine Zulu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic