May 24, 2017



Huku watani wao wakisubiria majibu kutoka Fifa, Yanga imesema kuwa haitavunja kambi ya wachezaji wake kwa ajili ya kulitembeza Kombe la Ligi Kuu Bara.

Yanga walitwaa taji hilo la ubingwa kwa mara 27 wikiendi iliyopita baada ya kufikisha pointi 68 sawa na Simba waliopitwa kwa idadi ya mabao ya kufunga kwenye msimu huu wa ligi kuu.

Simba hivi karibuni imedai kupeleka barua Fifa ikilalamikia kurudishiwa pointi zake ilizonyang’anywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Kagera Sugar kumchezesha beki wa kati Mohammed Fakhi anayedaiwa kuwa na kadi tatu za njano.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alisema lengo la kulitembeza kombe hilo mikoani ni kutoa shukrani kwa mashabiki wake waliopo huko.

“Tumeweka mipango yetu vizuri, tutalipeleka kombe letu Dodoma ili wanachama wetu na wabunge wenye mapenzi na Yanga SC walione kombe letu ambalo tumelichukua mara tatu mfululizo.

“Awali, tulipanga kucheza mechi moja Dodoma lakini uwanja umefungwa hivyo tutawaonyesha na kuondoka kuelekea mkoani Arusha.


“Tutavunja rasmi kambi mkoani Arusha baada ya kucheza mechi mbili za kirafiki na kuwapa fursa wapenzi na wanachama wetu jijini humo kuliona kombe lao,” alisema Mkwasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic