June 9, 2017



Beki Shomari Kapombe amesema alikaribia kusaini Simba kabla kuingia kambini timu ya taifa, Taifa Stars iliyosafiri hadi Misri.

Lakini akasisitiza, Azam FC ambayo ndiyo timu yake kwa sasa inaonekana ina nia ya kumbakiza Chamazi baada ya kuanzisha mazungumzo mapya.

Aliongeza kuwa, wakati akiwa kwenye hatua za mwisho za kusaini Simba, uongozi wa Azam nao umeanza mazungumzo naye kwa ajili ya kumbakiza kwenye kikosi cha timu hiyo.

"Nikiri kabisa ni kweli mimi nilifanya mazungumzo na viongozi wa Simba na aliyenifuata kwa ajili ya mazungumzo ni (Evans) Aveva na kikubwa ameniambia ananihitaji kwa ajili ya kunisajili.

“Katika mazungumzo huyo tulifikia makubaliano ya awali ya kusaini mkataba lakini kikubwa kilichonizuia nisisaini mkataba huo ni kambi ya Taifa Stars na ile presha yao ya Kombe la FA.


"Ninaamini mara baada ya ligi kuu kumalizika na mimi tuvunja kambi ya Stars, basi tutafikia muafaka mzuri wa mimi kusaini, lakini pia Azam nao wameonyesha nia ya kunibakiza, hivyo mazungumzo yanaendelea,” alisema Kapombe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic