Kocha wa mabingwa wa Ligi Kuu England, Antonio Conte amemuandikia ujumbe mshambuliaji wake, Diego Costa kuwa hamhitaji.
Awali ilionekana Costa angeweza kurejea Atletico Madrid lakini sasa wamezuiwa kusajili.
Costa raia wa Hispania ndiye aliyetoa siri hiyo wakati akihojiwa na kusema Conte kamuambia hamhitaji.
“Kaniandikia ujumbe, kasema hanihitaji, hajanijumuisha katika mipango ya msimu ujao,” alisema Costa raia wa Hispania.
Kocha huyo Muitaliano anaonekana kuelekeza nguvu zake kwa mshambulizi Romelu Lukaku kutoka Everton.
0 COMMENTS:
Post a Comment